Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Waandishi wa habari wapongezwa kufikisha ujumbe wa matumaini kwa watanzania juu ya mtazamo wa Iringa mpya katika maendeleo.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake siku tano ya kutembelea Tarafa tano za Wilaya ya Mufindi katika ukumbi wa mikitano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi jana.
Mhe Hapi alisema “nawashukuru sana waandishi wa habari. Timu yangu ya waandishi wa habari imefanya kazi kubwa sana. Kupitia vyombo vya habari tumetuma ujumbe wa matumaini kuwa Iringa inakwenda kubadilika na mambo yanakwenda kuwa mazuri”. Kupitia kampeni hii watu wengi watakuja kuwekeza Iringa, aliongeza. Uwekezaji utakapo ongezeka maana yake utatengeneza ajira nyingi kwa vijana na kukuza uchumi wa mkoa na pato la Taifa kuongezeka, alisisitiza. Kupitia vyombo vya habari mkoa utapata watalii wengi sana ambao wataendelea kukuza uchumi wa Mkoa wa Iringa.
Akiwa wilayani Mufindi, Mkuu wa Mkoa alitembelea Tarafa za Kibengu, Kasanga, Sadani, Malangali na Ifwagi. Pamoja na mambo mengine, alifanya mikutano mikubwa mitano ukiwemo mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Iringa mpya na mikutano midogo midogo 12 na wananchi kupewa fursa ya kuhoji na wataalam kujibu kero za wananchi.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.