Mkuu wa Mkoa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi aongoza jopo la TAKUKURU kukabidhi magari ya wananchi walioporwa kwa misingi ya dhuluma tarehe Mei 07, 2020.
Mheshiwa Hapi amekabidhi magari hayo kwa wananchi ambao walikopa fedha katika taasisi (SACCOS) ambazo si halali na kusababisha wananchi kushindwa kulipa mikopo kwa kuwazidishia riba na hatimaye kuonekana mkopo haumaliziki na kupelekea kuporwa mali zao.
Akiongea na Wanahabari leo Mheshimiwa Hapi amesema, wananchi wanahitaji fedha kutoka Taasisi mbalimbali za kukopesha, lakini kuna watu wameibuka na kuvunja sheria za nchi na kukopesha bila kufuata sheria, na sehemu kubwa ya mikopo hii haieleweki riba zake zinakokotolewa vipi. Serikali imekuwa imepambana na jambo hili kwa muda mrefu sasa. Wapo wakopeshaji hadi wanachukua kadi za benki kutoka kwa watumishi waliokopa. Mtu anaweza kumaliza mkopo lakini anaambiwa bado deni halijaisha.Hivi karibuni kumekuwa na uhujumu uchumi kupitia vyama mbalimbali vya ushirika, mwanachama anakopa na hataki kurejesha mkopo.
Leo nasimama hapa kueleza wenzetu TAKUKURU walivyofanya kazi nzuri kuweza kuwabana na kurejesha mikopo na magari yaliyoporwa kwa wananchi ambao walikopa fedha za moto. Magari hayo ni fuso lenye namba T 165 BLW na Toyota Serena (Noah) lenye namba T 311 DDF ambayo yaliporwa tangu mwaka 2017.
Mheshimiwa Hapi aliendelea kusema, ninawahakikishia wananchi kuwa sisi viongozi tuna dhamana kubwa ya kusaidia wananchi katika matatizo yao. Tumerejesha mali za awananchi ambazo zimeporwa kupitia minada feki, mikopo ya moto. Pia kiasi cha Shilingi 3.4 bilioni zimeokolewa kutoka kwa watu waliokopa kwenye vyama mbalimbali vya ushirika na kushindwa kurejesha. Nawasihi wananchi kuwa makini katika fedha za moto.
Naye Mkuu wa TAKUKURU Iringa ameeliza kuwa wanaendelea na ufuatiliaji wa madeni katika operasheni ili kuweza kuokoa fedha zaidi na kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali.
Pia mwananchi Mwalimu mstaafu (Bi Hadija Mazola) aliyeporwa gari kwa kukopa kiasi cha shilingi milioni mbili na akaweza kulipa kiasi cha shilingi milioni nne, lakini baadaye wakamuambia anadaiwa kiashi cha shilingi milioni nane. Aliposhindwa kulipa deni hilo ndipo akaporwa gari hiyo.
Nao wananchi walioporwa magari hayo waliishukuru Serikali na kuwapongeza kwa kazi wanazofanya. Kwani hawakutegemea kama magari yao yangerejea.
Imetolewa na:
Ofisi ya Habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.