Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi kuanza ziara yake kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika Tarafa ya Mahenge ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa Wilayani Kilolo.
Katika ziara hiyo, Mhe Hapi atatembelea na kukagua hifadhi asilia ya Kilombero, kutembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari Nyanzwa na kumalizia kwa mkutano wa hadhara pamoja na kusikiza kero za wananchi maarufu (mahakama ya wananchi) ambazo zitajibiwa na wataalam wa kisekta.
Mkuu wa Mkoa yupo siku ya tatu ya ziara yake ya siku nne kutembelea Tarafa tatu za Wilaya ya Kilolo na kufanya majumuisho ya ziara nzima siku ya nne.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.