RC - QUEEN "SITAKUJA KUFANYA ZIARA ZA KUSHITUKIZA"
MKUU Wa Mkoa Wa Iringa Queen Sendiga, amewataka watumishi wa sekta ya afya kufanya kazi kwa uadirifu bila kushurutishwa, huku akisema katika uongozi wake hatakuja kufanya ziara za kushitukiza bali atataka kila mfanyakazi wa umma kujua wajibu wake akiwa mahala pake pa kazi
Hayo aliyasema jana wakati wa ziara ya kukagua ufanisi wa kazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa
Alisema endapo kila mmoja atajua wajibu na majukumu yake hakuna haja ya kushitukizana ,na ndio maana alienda akiwa ametoa taarifa kwamba anaenda ila itakapo bidi atafanya hivyo
"Mnaweza mkajiuliza mbona mkuu huyu hatumii ziara za kushitukiza kama wengine ambao wakifika wanakimbizana kwenye habari ya kufanya ziara kwa kushitukiza, niseme tu sisi wote ni watumishi wa umma ile habari ya kwenda mahali na kuaza kukurupushana kwangu naona kama haina tija ,"alisema Mkuu wa mkoa
Aidha alimuagiza mganga mkuu kuwashughurikia wahudumu wote ambao hawatoi huduma ipasavyo kukaa nao na kuwaambia wajirekebishe na kama hawawezi wanaona taaruma waliyoisomea hawakujua itakuwa na majukumu makubwa waache wakafanye kazi nyingine
Pia aliwaomba watumishi wote wawe na maadili katika kazi zao kwani hatakuwa tayari kupokea malalamiko ya aina yoyote yale kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji kazi wa wahudumu
"Najua kwamba kuna, upungufu wawauguzi lakini isiwe sababu ya kushidwa kufanya kazi kwani ndio kazi tuliyopewa tuifanye kwa moyo wote, alisema Queen.
Queen alisema matarajio na mategemeo yake makubwa ni kuziboresha huduma za afya ili kuwasaidia wananchi.
Aidha amesema anajua kuwa sekta ya afya inachangamoto na tayari amekaa na viongozi wamemueleza mambo yote na anafanya kila namna kuhakikisha anazishughulikia
"Hivi karibuni nategemea kwenda Dodoma nitahakikisha nakutana na viongozi wa sekta husika ya wizara ya afya ili kuona wanatusaidiaje hata kwa hela kidogo tuliyonayo tuweze kupatiwa mahitaji yetu" alisema Aliendelea kusema, nimesikia tatizo la upungufu ya wataalamu bingwa wa magonjwa mbalimbali hivyo nitaongea na waganga wa mkoa ili waorodheshe changamoto zote ili zikitoka fursa za ajira tuone na sisi wanatusaidiaje ,"alisema Queen
Pia alisema ameridhishwa na utoaji huduma wa hospitali hiyo pamoja na watendaji wake namna wanavyo wajibika licha ya hayo pia alisema kumekuwa na baadhi ya wahudumu kutumia lugha chafu kwa wagonjwa na kuwataka kuacha maramoja kwani kazi hiyo ni wito kama zilivo kazi nyingine
Alisema maadili ya wauguzi ni tofauti na maadili ya kazi nyingine hivyo kashifa, chuki, majibu yasiyoridhisha na vikwanzo vya aina yeyote havitakiwi kwa wauguzi
"Ningumu kumtambua mtu mwenye tabia hizo kwasababu ya wingi wenu hivyo lazima ujichunge mwenyewe na kwakuwa kuna viongozi tutazidi kukumbushana,"alisema
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.