Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe:Queen Cuthbert Sendiga amefanya ziara katika hospitali ya Frelimo iliyopo ndani ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kukagua huduma ambazo zinatolewa hospitalini hapo na ametoa maagizo ya kuongezwa kwa wahudumu wanaotoa huduma ya chanjo na kupima ili kupunguza foleni isiyo ya lazima,
"ile foleni ya kinamama vile hapana si sawa, ule mrundikano wa wakinamama wanaopata huduma ya chanjo na kupima jumatatu na alhamisi sitaki kuuona" Rc Sendiga
Aidha Mhe: Queen Sendiga ametaka kuongezwa kwa kasi ya ujenzi wa wodi ya kinamama na kinababa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati, ambapo kwa mujibu wa makubaliano miradi hiyo inatakiwa kukamilika ifikapo mwezi April mwaka huu 2022.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.