Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewaagiza wanaosimama ujenzi wa miradi kuhakikisha wanaongeza mafundi wa kujenga katika miradi hiyo ili kukamilisha miradi kwa wakati.
Ameyasema hayo leo wakati aKifanya ziara ya kukagua miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo ametembelea katika shule ya msingi Kiwere, Shule ya Sekondari Kiwere, Shule ya msingi Itagutwa, shule ya Sekondari Furahisha na shule ya Sekondari ya Ismani ambapo amekagua na kuwataka wasimamizi wa maradi hiyo kumaliza miradi kwa wakati
Akiwa katika shule ya msingi ya Kiwere ambapo kuna mradi wa ujenzi wa vyoo amempa wiki tatu msimamizi wa jengo hilo kwanza kuhakikisha anaongeza mafundi na kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo kwa wakati nakama atashindwa basi kazi atapewa mtu mwingine ambaye atamaliza mradi huo kwa wakati.
Pia akiwa katika shule ya Msingi Itagutwa ambayo ina mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi moja unaogharimu kiasi cha Shilingi Million 40 amemtaka msimamizi wa jengo hilo kukamilisha mradi kwa wakati ili Watoto waanze kuyatumia madarasa hayo.
Nao baadhi ya wazazi na wananchi kutoka katika kata ya Itagutwa wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa majengo hayo ambapo wamesema kutokana na madarasa yaliyopo kuwa ni mabovu basi madarasa hayo mapya yatakuwa mkombozi kwa wanafunzi hao.
Sambamba na hayo Mhe. Serukamba amepongeza kasi ya ujenzi wa madarasa na vyoo inayoendelea katika shule ya sekondari Kiwere, Ismani na Shule ya Sekondari ya Furaha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.