Baada ya Skimu kubwa ya umwagiliaji ya mkombozi kufikia mwisho,Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka Viongozi wa Wilaya,kijiji Pamoja na Maafisa Ardhi kwenda kutatua migogoro yote ya Ardhi katika Tarafa ya pawaga ili eneo Hilo liwe mfano kwenye umwagiliaji Nchini, Kwa kutambua wamiliki wa mashamba ili kuhakikisha kila mwenye eneo ana hati ya Ardhi.
Ameyasema Hayo Septemba 6, 2024 wakati wa Majadiliano ya skimu ya umwagiliaji ya mkombozi
Mbali na hayo, Mhe. Serukamba ametoa agizo kwa wenyekiti wa vijiji waende wakaitishe mkutano kwa wananchi ili wapewe na Kila mmoja aweze kutambua mipaka ya ardhi yake.
Akihitimisha kikao hicho, mhe.Serukamba amemuagiza Mkuu wa wilaya na Afisa tarafa kusimamia zoezi hilo na baada ya wiki mbili waweze kurejesha mrejesho wa zoezi hilo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.