Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na wadau wa maendeleo katika kuongezea mahali ambapo serikali inaishia katika kuwahudumia wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa mganga mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dr Atupele Mwandiga alipokuwa akifunga kikao cha kuutambulisha mradi wa ‘USAID Tulonge Afya’ kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa jana.
Dr Mwandiga alisema kuwa wadau wa maedeleo wamekuwa msaada mkubwa katika kuchangia juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wake. “Wadau wa maendeleo wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana katika kuwaletea maendeleo na kuboresha afya za wananchi wetu. Uwepo wenu katika Mkoa huu umeongeza kasi ya serikali ya Mkoa na Halmashauri zake ya kuwafikia wananchi katika jitihada zao mbalimbali za kukabiliana na changamoto za maisha, hasa kujikwamua kiuchumi na kuimarisha afya zao” alisema Dr Mwandiga.
Dr Mwandiga aliwapongeza waandaaji wa mradi huo kwa kuchagua kutumia mbinu za mabadiliko ya tabia kwa wanajamii (SBCC). Alisema kuwa mbinu hiyo imekuwa ikitoa matokeo chanya inapotumika vizuri.
Dr Mwandiga aliwaagiza waganga wakuu wa Wilaya kusimamia vizuri na kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo kupitia mbinu za mabadiliko ya tabia kwa wanajaamii.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.