Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mamlaka za serikali za mitaa na wadau wa maendeleo wametakiwa kuwatumia maafisa habari wa serikali katika kuhabarisha utekelezaji wa miradi ili wananchi waweze kunufaika na huduma zao.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr Atupele Mwandiga alipokuwa akifunga kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa wadau wa Mkoa wa Iringa katika hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa jana.
Dr Mwandiga alisema kuwa mafanikio ya miradi inayotekelezwa kwa wananchi yanategemea na utoaji na upatikanaji wa taarifa za huduma zinazotolewa. “Vivyo, hivyo mafanikio ya mradi huu wa ‘USAID Tulonge Afya’ pamoja na mambo mengine utategemea sana upatikanaji na ubadilishanaji wa taarifa za huduma na mafanikio. Na hili ni jukumu la maafisa habari wa serikali. Bahati nzuri kwa Mkoa wetu wa Iringa, serikali imeajiri maafisa habari katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote. Ni matumaini yangu kuwa wataalamu hawa watatumika vizuri katika kufikia malengo ya mradi huu” alisema Dr Mwandiga. Aidha, aliwataka kuwatumia pia maafisa maendeleo ya jamii walio katika kata zote za Mkoa wa Iringa katika kutekeleza mradi huo.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.