Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe, Halima Dendego ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa ameambatana na wajumbe wa kamati hiyo amewatoa hofu wananchi wa kijiji cha tanangozi kutokana na taharuki ya uwepo wa simba wanakula mifugo yao na kutishia maisha yao.
Mhe, Mkuu wa Mkoa amesema jambo hilo linafanyiwa kazi na zoezi la kuwatafuta simba hao linaendelea hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hao.
"Mhe, Dendego amesema naomba wananchi mshiriki kutoa taarifa tu na kazi ya kuwatafuta na kuwakamata waachieni wataalamu wa wanyamapori"
Kwa upande wake Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Godwell Ole Meing'ataki amewataka wananchi kuwa watulivu kwani wamejipanga kuhakikisha wanawapata simba hao haraka iwezekanavyo kabla awajaleta madahara Kwa binadamu.
Pi amewatahadharisha wananchi kuto kula mabaki ya mifugo hiyo Kwa katika zoezi la kuwakamata Simba hao wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutumia madawa ya usingizi Kwa kuweka kwenye masalia ya mifugo hiyo Kwa sababu Simba ana tabia ya kula na kubakiza mzoga na Kisha anarudia tena.
Imetolewa na Afisa habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.