Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima dendego wakati akikabidhi Pikipiki kwa maafisa ugani wa Halmashauri zote ziliopo mkoani humo huku akiwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa nguvu zote ili kukuza uchumi wa Nchi.
Akizungumza na Maafisa Ugani hao leo 28/02/2023 Mhe.Dendego amesema kuwa kutokana na changamoto kadha wa kadha zilizokuwa zikiwakumba maafisa hao kubwa ikiwa ni suala la usafiri jambo ambalo lilipelekea wakulima kutokufikiwa kwa wakati na kukwamisha uzalishaji wa mazao kwa sasa kilio hicho kimekwishwa baada ya kukabidhiwa pikipiki na kwa sasa uchumi wa mkoa wa Iringa utazidi kukua.
“lakini hatuwezi kulima kilimo bora kama wakulima wetu walio wengi wale wa chini awatapata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa Ugani kwahiyo leo tunapoenda kugawa hizi pikipiki ndugu zangu ninaomba sana tuweke mkataba leo mimi nitazigawa kwa maelekezo ya kugawa lakini kuna hatua ya pili tutasainiana mikataba kama maafisa ugani na ofisi yangu ya mkoa na wilaya nione pikipiki hizi zinaenda kubadirisha kilimo chetu tunataka kuona mapinduzi ya kijani katika mkoa wa Iringa”
Eng. Ndugu Leonard Masanja ni katibu Tawala Mkoa wa Iringa amewasisitiza maafisa Ugani hao kufanya kazi kwa bidii kuhakikisga wanawafikia wakulima wote katika maeneo yao na kuwapa elimu iliyo sahihi na huku wakitumia vyombo hivyo kama ilivyopangwa.
Awali akitoa taarifa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ndugu Elias Luvanda amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa Iringa umepokea pikipiki 216 kwaajili ya maafisa ugani na pia Mkoa umepokea Pawatila moja kwaajili ya kusaidia Ugani ili kukuza sekta hiyo ya kilimoWakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo maafisa ugani hao wametoa shukrani na pongezi kwa serikali kwa kuwaletea vitendea kazi hivyo huku wakiahidi kuwahudumia wananchi wote waliopo katika maeneo yao.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.