Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Halima Dendego amewafahamisha wananchi wa Mkoa wa Iringa kuwepo kwa ugeni wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaetarajiwa kupokelewa katika Mkoa wa Iringa tarehe 11 Agosti,2022.
Mheshimiwa Rais atakuwa na ziara ya kikazi hadi tarehe 13 Agosti, 2022 na katika ziara hiyo anatarajia kukagua shughuli za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Mkoa wa Iringa kama ifuatavyo:
Tarehe 11/08/2022 Mheshimiwa Rais atapokelewa na uongozi wa Mkoa katika eneo la Nyororo Wilayani Mufindi ambapo atasalimia wananchi na baada ya hapo ataelekea katika Kijiji cha sawala ambako ataweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Lami Sawala-Iyegea yenye urefu wa 30.3 Km. Akiwa katika eneo hilo la mradi pia atawasalimia Wananchi.
Mhe.Rais ataondoka Sawala kuelekea Ikulu ndogo Iringa. Akiwa njiani, atapata fursa ya kusalimia wananchi katika maeneo ya Mafinga Mji na Ifunda.
Aidha, jioni atazungumza na wazee.
Tarehe 12/08/2022 Mheshimiwa Rais atafanya shughuli zifuatazo:
Ataweka Jiwe la Msinga katika Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Iringa na atasalimia Wananchi katika eneo hilo.
Vilevile, siku hii atahutubia wananchi katika mkutano wa Hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Samora Mjini Iringa.
Tarehe 13/08/2022 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahitimisha ziara yake katika Mkoa wa Iringa na kuondoka kuelekea Dodoma. Aidha, atakapokuwa njiani, atasimama Isimani Tarafani kwaajili ya kusalimia wananchi.
Hivyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego anatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi sana na kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, katika maeneo ambayo atasalimia wananchi, ataweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa wa Iringa na kushiriki mkutano wa hadhara tarehe 12 Agosti,2022.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.