Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Watekelezaji wa mradi wa USAID Tulonge Afya wametakiwa kutumia fedha za utekelezaji kwa mujibu wa taratibu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hills iliyopo mjini Iringa jana.
Ayubu alisema kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinatolewa na serikili ya Marekani kupitia shirika la maendeleo la Marekani USAID. “Naomba fedha hizi zikatumike kwa kufuata utaratibu ili kufanikisha kufikia malengo yake. Nataka niwakumbushe kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu katika kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za wadau wa maendeleo na za serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa thamani ya fedha kwenye miradi ya maendeleo inazingatiwa na watekelezaji” alisema Ayubu.
Alisema kuwa mradi huo unalenga kuhamasisha wanajamii kutumia huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya afya. “Ninawahakikishia kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana nanyi katika uboreshaji wa huduma ili wananchi wakishahamasika waweze kwenda vituoni na kupata huduma zilizo bora” alisema Ayubu.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.