Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Iringa kwa kuwajali na kuwaenzi wazee na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya jamii.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo October 03, 2023 mara baada ya kupokelewa na Viongozi Mbalimbali na Wananchi wa Mkoa wa Iringa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Dkt. Biteko amesema kuwa katika jamii yoyote ile wazee ni watu wa muhimu katika mambo mbalimbali .
"Naongea kama mtu niliyefundishwa dini na sio kama kiongozi wa dini hivyo niwaambie tu viongozi wa Mkoa wa Iringa mtabarikiwa ," amesema Dkt Biteko.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.