Baada ya Agizo alilolitoa hapo jana Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba akiwa kwenye baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mafinga la kumtaka Mkurugenzi kusimamia ubomoaji wa vibanda 331 katika soko la mafinga kutoka na kitendo cha wafanyabiashara wa soko hilo kushindwa kutekeleza agizo la kusaini mkataba ndani ndani ya siku 20, Kufuatia agizo hilo uongozi wa wafanyabiashara ulilazimika kukutana na Mkuu wa Mkoa na kufanya nae mazungumzo na kumwomba kusitisha uamuzo huo wa kubomoa vibanda na badala yake azungumze na wafanyabiashara wote ili kufikia makubaliano ya pamoja jambo ambalo limetekelezwa huku Mkuu wa Mkoa akiwataka wafanyabiashara kusaini mkataba hadi kufikia jumatatu ya mei 27,2024 huku wakitakiwa kuanza kulipa kiasi cha shilingi Elfu 80 kwa mwezi kwa kila kibanda makubaliano ambayo utekelezaji wake utaanza juni mosi mwaka huu.Awali wafanyabiashara hao walikuwa wakilipa kati ya shilingi elfu tatu mpaka elfu tisa kwa mwezi jambo lililoikosesha mapato Halmashauri ya mji wa Mafinga na kuibua mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka 15 huku Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba akitumia siku 21 kumaliza mgogoro huo jambo lililowafurahisha wafanyabiashara hao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.