Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala kuwafatilia wakandarasi wazembe ambao hawatamaliza miradi kwa wakati na kuwachukulia hatua za kisheria.
Agizo hilo amelitoa Mei 21, 2024, baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa akiwa amengozana na Katibu Tawala Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komredi Kheri James, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada, pamoja na viongozi mbalimbali.
Akiongea na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ujenzi, Wananchi na baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya Kata Mhe, Serukamba amesema anawashukuru kwa kujitokeza katika ziara hiyo, pia kwa ushiriki wa miradi inayotekelezwa na kuwataka wakandarasi pamoja na mafundi waongeze kasi ya ujenzi ili miradi hiyo ikamilike kufikia mwisho wa mwezi Juni 2024.
"Nawapongeza sana kujitokeza kwa wingi, pia nawapongeza kwa ushiriki wa ujenzi wa miradi hii, Mhe Rais Ana nia njema na anawapenda ndiyo maana anawaletea fedha za ujenzi wa miradi hii, mimi kazi yangu ni moja tu nimekuja kuongea na mafundi kuongeza kasi ili kufikia mwisho wa mwezi June mwaka huu miradi iwe imekamilika." Amesema Serukamba.
Miradi iliyotembelewa ni miradi ya Sekta ya Elimu na Afya, huku lengo likiwa ni kuona maendeleo ya miradi hiyo na changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.