Dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Wakulima wa mazao nchini wanazidi kunufaika na harakati za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha inatatua changamoto na kuwawezesha wakulima hao katika kila hali Katika Mkoa wa Iringa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kufanya mambo makubwa katika sekata ya kilimo ambapo katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo wakulima 1700 watanufaika na skimu ya umwagiliaji ya Mgambalenga baada ya kukamilika kwa ujenzi wa skimu hiyo,
Akitoa historia ya skimu hiyo Diwani wa Kata ya Ruaha mbuyuni Mhe. Rashid Nzelemela amesema skimu hiyo imeanza kujengwa tangu mwaka 2014 ambapo Serikali ilitoa fedha lakini bado hazikutosheleza kukamilisha mradi huo hivyo kupitia tume ya umwagiliaji kwa sasa shilingi Billioni 20 zinatolewa ili kukamilisha mradi huo jambo ambalo litalifungua eneo hilo ambalo ni maarufu kwa ulimaji wa Nyanya na vitunguu Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Anna Msola amesema mradi huo wa Mgambalenga pindi utakapokamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi na utaleta na kukuza uchumi katika halmashauri ya wilaya ya kilolo Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amepongeza kasi iliyopo lakini pia ameendelea kuomba kwa tume ya umwagiliaji na wizara ya kilimo kuwafikishia kwa haraka hizo fedha ili waweze kuukamilisha mradi huo kwani mradi huo utatokomeza umaskini kwa wakazi hao Skimu hiyo ya umwagiliaji ya Mgambalenga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, vijiji vipatavyo vitatu vitanufaika na skimu hiyo ambavyo ni Mtandika, Msosa na Ruaha Mbuyuni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.