WAKUU WA WILAYA WAPYA IRINGA WAAPA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA MUUNGOZO WA ILANI YA CCM
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga, siku ya leo Juni 21. 2021 amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya wawili wa Iringa na Mufindi katika ukumbi wa Mikutano wa Siasa na Kilimo, na Mkuu wa Wilaya ya kilolo yeye ameapa kiapo cha maadili kwa sababu amebadilishiwa kituo cha kazi.
Uwapisho huo umefanyioka mara baada ya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wa nchi nzima uliofanywa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu siku ya Jumamosi tarehe 19.06.2021
Majina ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Iringa walioapishwa ni pamoja na Mhe. Mohamed Moyo, (Mkuu wa Wilaya ya Iringa), Mhe. Saady Mtambule (Mkuu wa wilaya ya Mufindi), na Mhe. Peres Magiri (Mkuu wa Wilaya ya Kilolo)
Aidha mara baada ya kuapishwa kwao, akizungumza mbele ya Wakuu hao wa Wilaya,
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen amewataka viongozi hao kwenda kutumika kwa manufaa ya Wananchi kupitia kutatua changamoto zote zinazowakumba pamoja na kusimamia vyema miradi ya maendeleo katika kila maeneo yao ya kazi
“hakikisheni mnatenda haki bila upendeleo wowote, bila kubagua dini wala kabila kwani Tanzania ni ya watu wote na wote ni sawa, hivyo msitumie madaraka yenu kuwaonea wengine” Mhe. Queen amesema
Mwisho, viongozi hao wameahidi mbele ya Mkuu wa Mkoa kwenda kusimama na kutekeleza majumu yao kama ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyowataka kutumika, Alisema Mhe. Saady Mtambule kwa niaba ya wakuu wa Wilaya walioapishwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.