Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa mkoani Iringa watakiwa kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Rais ya utoaji wa elimu bila malipo mkoani hapa.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiongea na walimu wakuu na wakuu wa shule katika kikao maalum cha kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo ya Rais juu ya elimu bila malipo kilichofanyika katika shule ya sekondari Lugalo leo.
“Niwaagize wakuu wa Wilaya kama yapo mambo kama hayo yanaendelea katika Wilaya zenu na nyie hamjui na hamjaniambia nayie mtakuwa mnanihujimu. Sasa nisingependa tabia ya kuhujumiana ikawa sehemu ya utawala katika Mkoa wetu” alisema Masenza.
Aidha, aliwataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikalai za Mitaa kusimamia shule katika Halmashauri zao ili suala la uchangishaji michango kinyume na maelekezo usiwepo.
Alisema kuwa kikao hicho ni kikao cha kujiridhisha kama kuna shule inayoendesha michango na inasimamiwa na mwalimu. Alisema kuwa mwisho wa kikao hicho kila mkuu wa shule awe ameandika barua kumueleza mkuu wa Mkoa juu ya hali ya jambo hilo.
Aidha, mkuu wa Mkoa aliagiza kuwa kwenye elimu bure hakuna michango, na kupiga marufuku kwa mwalimu yeyote kuchangisha mchango na kuwarudisha nyumbani wanafunzi kwa kisingizio cha michango. Aidha, alipiga marufuku wanafunzi wote wanaoripoti shuleni kurudishwa nyumbani kwa kutokuwa na sare.
Wakati huohuo, amezitaka shule binafsi kuacha mara moja kukaririsha vidato wanafunzi wasiofikia wastani na kwamba shule zitakazokiuka agizo hilo zitafutiwa usajili.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.