Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wanafunzi nchini wametakiwa kusoma kwa bidhii ili kuunga mkono uwekezaji wa serikali katika sekta ya elimu ili ichangie katika uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo iliyolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika sekondari ya Igombavanu wilayani Mufindi.
Kabeho alisema kuwa serikali imeondoa ada na michango shuleni ambayo ilikuwa ni kero kwa wananchi ili wanafunzi wengi waweze kufurahia haki ya kupata elimu. Alisema kuwa elimu ni muhimu sana kwa jamii katika utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kuelekea uchumi wa viwanda mwaka 2025. “Uchumi wa viwanda unategea sana uwekezaji katika elimu. Serikali ya awamu ya tano kwa kuona umuhimu huo, iliamua kutoa elimu bila malipo ili watanzania wote wapate elimu hiyo msingi” alisema Kabeho. Aidha, aliongeza kuwa serikali imedhamiria kuboresha elimu kaunzia ya awali hadi elimu ya juu. Uboreshaji wa sekta ya elimu nchini unakwenda pamoja na ukuaji wa elimu ya ufundi na ufundi stadi kwa kuweka msisitizo katika maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu, aliongeza.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.