Ikiwa ni siku ya nne ya ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ya kukagua,kuzindua miradi Oktoba 1, 2024. ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za Kilolo Mjini kwa kiwango cha lami.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, Waziri Ulega amesema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuimarisha huduma za jamii kwa kujenga miundombinu mbalimbali ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa wepesi huku akiwataka wananchi kuiunga mkono Serikali kwa kutunza vyema miundombinu hiyo ili iwasaidie katika kujiletea maendeleo yao.
Katika hatua nyingine, Waziri Ulega ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Kilolo na kuzindua huduma katika majengo ya wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU), jengo la kuhifadhia maiti na kukagua shughuli za ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Lugalo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.