Na. ofisi ya mkuu wa mkoa
Watahiniwa zaidi ya 24,000 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017 mkoani Iringa.
Kauli hiyo ilitolewa na afisa elimu mkoa wa Iringa, mwalimu Majuto Njanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Iringa leo.
Mwalimu Njanga alisema “jumla ya idadi ya watahiniwa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017 kwa mkoa wa Iringa ni 24,906. Kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 11,494 na wasichana ni 13,412”. Akiongelea Mchanganuo kwa kila Halmashauri, alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ina watahiniwa (3,738), Halmashauri ya wilaya ya Iringa watahiniwa (6,519), Halmashauri ya wilaya ya Kilolo watahiniwa (5,940), Halmashauri ya wilaya ya Mufindi watahiniwa (6,820) na Halmashauri ya mji Mafinga watahiniwa (1,889).
Akiongelea mandalizi ya mitihani hiyo, afisa elimu mkoa wa Iringa alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika. Alisema kuwa maandalizi hayo yalitanguliwa na semina elekezi kwa wahusika wote. Alisema kuwa mitihani imesambazwa katika Halmashauri zote za mkoa wa Iringa. “Mitihani yote imekwishasambazwa kila Halmashauri na usalama ni mzuri, hakuna tatizo lolote lililoripotiwa. Kwa mkoa mzima kuna mikondo 1,162 ambayo ni sawa na idadi ya wasimamizi” alisema Mwalimu Njanga.
Mtihani wa kumaliza elimi ya msingi mwaka 2017 utaanza tarehe 6/9/2017 hadi 7/9/2017 nchini kote kwa kuanza na masomo ya lugha ya kiingereza, hisabati na maarifa ya jamii na siku ya mwisho kumalizia na mitihani ya sayansi na kiswahili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.