ZIARA YA MHE RC SENDIGA NA BI SENEDA, OFISINI KWA MHE WAZIRI GWAJIMA. 3/6/2021
Mhe Queen Sendiga, Mkuu wa Mkoa Iringa akiwa ameambatana na bi, Happynes Seneda Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, leo wamefanya ziara ya kikao kazi katika ofisi ya Mhe waziri wa Afya ambapo wamefanya mazungumzo ya sekta ya afya kwa lengo la kuboresha huduma kwenye hospitali zilizopo ndani ya Mkoa wa Iringa.
Mhe Gwajima Waziri wa afya kumekuwa na changamoto kubwa sana katika uendeshaji wa hospitali zetu kwa sababu kuna udanganyifu mkubwa sana hasa katika kununua dawa, bima ya afya pamoja na watumishi wa afya kufanya kazi sehemu mbili kwa maana ya serikali na hospitali binafsi hii inaondoa umakini kiutendaji na kupelekea baadhi ya watumishi hao kuwa na maduka yao na hospitali binafsi.
Mhe Gwajima, amesema kuwa hii vita siyo ndogo maana unapofatilia ubadhilifu huu kumbuka unagusa maslahi ya watu hivyo wako tayari hata kukuuwa.
Hata hivyo Mhe Gwajima Waziri wa afya, amesema kuwa amezipokea changamoto za Mkoa wa Iringa hivyo atahakikisha anapatikana daktari bingwa wa mifupa, magonjwa ya ndani na pua na koo, pia amewataka MSD wafike mara moja waende wakafunge vifaa vyote vya mashine za usingizi.
Mhe Sendiga, amemwambia Mhe waziri Gwajima kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana la ubakaji na ulawiti ndani ya Mkoa Iringa na ili linatoka na waganga wa jadi ambao siyo wahaminifu ( matapeli) wanawadanganya wateja wao kuwa ili wafanikiwe lazima wabake watoto ndio wafanikiwe, akitoa ufafanuzi bi, Seneda (RAS) amesema pindi jeshi la polisi linapowakamata waganga hao Mwenyekiti wa chama cha waganga wa jadi Taifa anapiga simu polisi na kuwataka wamuachie haraka sana mganga mwenzao kwani yupo kisheria.
Mhe Gwajima, amesema kuwa Kuna shida kubwa sana hapa ya kushughulikia ili tatizo maana awa waganga wa jadi wanekuwa wakiingilia mifumo ya serikali na kusababisha migogoro kwa jamii na serikali, hata hivyo amesema atakuja Iringa na kufanya kikao na KUU Iringa, viongozi wa jadi, amsema yeye amjitoa muhanga kwa lengo la kusaidia Taifa kwa ujumla. Nachukizwa sana na mabango ya waganga mitaani, pia Leo atakutana na Mhe Simbachawene kujadili juu ya hili tatizo la waganga wa jadi, mpaka Sasa Kuna vyama 14 wa waganga wa jadi hapa Nchini.
Mhe Sendiga, alimshukuru sana Mhe Gwajima kwa kikao kazi hicho ambacho kitaleta matokeo chanya kwenye Mkoa wa Iringa.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.