Katika ziara yake ya siku mbili tarehe 6-7/01/2020 Mkoani humu ametembelea kituo kilichoanzishwa kusaga unga wenye virutubisho ili kunusuru hali ya udumavu katika familia. Udumavu unasababisha kurudisha nyuma maendeleo ya familia hata nchi kwa ujumla, kwani mtu mwenye udumavu hawezi kukua kiakili na kimwili, ameyasema hayo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Ndugulile.
Mheshimiwa Ndugulile ametembelea sehemu mbalimbali kuangalia maendeleo ya hali ya afya na kuagiza unga utakaotumika kuanzia sasa ni ule wenye virutubisho. Utatumika mashuleni na nyumbani ili kunusuru watoto. Unga huo wenye virutubisho ni mzuri kwa watoto na mama mjamzito. Pia alipotembelea hospitali ya Rufaa Iringa, ameagiza kuwepo na jiko kwa ajili ya wazazi wanaosubiri kujifungua hii itasaidia kuwaagiza wazazi waje na chakula cha lishe kupikia hapo. Ameagiza elimu itolewe kwa wajasiriamali wanaoandaa unga ili waandae wenye virutubisho.
Mheshimiwa Ndugulie akiwa katika Kijiji cha Tanangozi alishiriki kuwapima watoto uzito, urefu na kuwanywesha uji wenye virutubisho ambao ulikuwa umeandaliwa na Watoa Huduma za Afya.
Mheshimiwa Ndugulile pia ameagiza NHIF kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfumo wa Bima kwa vifurushi, kwani katika kukagua kwake hakuridhika na uhamasishaji unaotolewa kwa wananchi.
Mheshimiwa pia ametembelea Kata ya Rungemba Wilayani Mufindi na kukagua maendeleo ya hali ya afya kwa wakazi wa Kata hiyo, pia Chuo cha Maendeleo ya Jamii na kuona maendeleo na changamoto za chuo hicho.
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Ndugulile ameagiza watumishi wote wa Idara ya Afya wawe wanavaa vitambulisho wakati wote wanapotoa huduma, huduma kwa wazee iboreshwe, huduma za dharura zitolewe ipasavyo na bila malipo yoyote wakati wa kutoa huduma hasa katika huduma za mama na mtoto.
Mheshimiwa Ndugulile pia amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuchangia maendeleo ya ujenzi wa baadhi ya majengo katika Hospitali ya Rufaa Mkoni humu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Habari Mkoa,
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.