Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Peter Serukamba awataka Wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa
Kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA,ambayo kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoani Iringa, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameongoza kikao cha kwa kwanza cha mashindano hayo kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa taasisi.
Akizungumza leo Machi,13,2025, kwenye kikao hicho Mhe. serukamba amewataka viongozi,wananchi na wafanyabiashara kujiaandaa kuwapokea wageni hawa kwanza kwa kutopandisha bei za bidhaa na nauli kwa upande wa usafiri.
Mhe. Serukamba ameeleza Mkoa wa Iringa umejipanga na utahakikisha Usalama wa washiriki na wageni ikiwemo maandalizi ya miundombinu itakayotumika Pamoja na huduma zitakazotolewa kwa washiriki.
Mashindano haya yanatarajia kufanyika Juni,08-Julai 04, 2025 mkoani Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.