Ikiwa ni wiki la Maadhimisho ya Usafi wa Mazingira Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Halima O. Dendego akiwa ameambatana na Viongozi wa Afya amezindua Zahanati ya Itagutwa Iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Kata ya Kiwele na Kutembelea Shule Ya Msingi Kitapilimwa Kutazama Ujenzi Wa Vyoo Vilivyojenga na Jumuiya ya Uandisi na Uifadhi wa Mazingira EEPCO kwa kusaidiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa ufadhili wa UNICEFAkitoa taarifa ya Ujenzi wa Zahanati hiyo Mwakilishi wa EEPCO amesema kuwa shirika hilo lilipokea kiasi cha shilingi Bilioni Nne na Hamsini na hamsini na Nane na Mia Nane Kumi na Tano na Mianne Hamsini kutoka UNICEF ikiwa na lengo la kutekeleza miradi yam aji, Shule na Ujenzi wa Vituo vya Afya pia amesema lengo kuu la EEPCO ni kushirikiana na Serikali na Taasisi mbalimbali Duniani ili kuboresha uelewa na kujifunza mikakati mbalimbali ya kuhifadhi mazingira ni kutatua changamoto ya Mazingira mashuleni na katika vituo vya Afya.Akizindua Zahanati hiyo Mhe Halima Dendego ametoa shukurani kwa EEPCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya Kujitolea kuipambania jamii katika kujenga Zahanati, kujenga Vyoo katika shule na kazi nyingine wanazozifanya huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kujitokeza katika kuleta maendeleo kwenye jamii kwa kujitolea katika ujenzi wa Shule na Zahanati na kutunza Miundombinu ambayo imeboreshwa na Shirika hilo na kuwa ahidi kuwa serikali ipo Pamoja nao katika kila jambo watakalotaka kulifanya.Pia Akiwa Katika Shule ya Msingi Kitapilimwa Mhe. Dendego amewapongeza wananchi wa eneo hilo kwa namna wanavyojitoa katika kwenye maendeleo ya elimu na kuwaahidi kuwa serikali ipo Pamoja nao kama Mkuu wa Mkoa atahakikisha wanashirikiana bega kwa bega katika kuboresha miundombinu ya shule hizo.Nao baadhi ya wananchi wametoa shukrani kwa serikali huku wakiwapongeza wauguzi waliopo katika zahanati hiyo kwa namna wanavyofanya kazi
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa amefanya uzinduzi wa kikao cha kupokea maagizo ya Miongozo Mitatu ya Kuboresha Elimu ya Misingi na Sekondari uliotolewa Agosti mwaka huu Mkoani Tabora na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Shule ya wasichana Iringa.(Iringa gilrs) Katika uzinduzi huo Mhe Halima Dendego amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya huku akiwaahidi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha walimu wanapatiwa haki zao za msingi na wanawajibika katika kutoa Elimu Bora. Aidha Mhe. Halima Dendego amesema “Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kila mwaka tutakuwa tunaandaa kikao cha tathimini kwa sekta ya Elimu ili tuweza kuona mafanikio,changamoto na mambo yanayofuata siku za mbele tuweza kuyakabiliwa kwa Pamoja”
Mhe Queen Sendiga akitoa maelezo ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya Mkoa wa Iringa upande wa Barabara (TARURA na TANROADS) ndani ya kipindi cha mwaka mmoja cha Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.