Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Katibu Tawala na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kukutana na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijajini na Mijini TARURA kuzungumza nae kwaajili ya Ujenzi wa barabara iendayo katika kituo cha Afya cha wenda kinachomilikiwa na kanisa la Katoliki Jimbo la Iringa.
Hayo yamejiri wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa jengo la upasuaji mkubwa lililopo katika kituo hicho.
Akitoa taarifa ya kituo hicho mganga mfawidhi wa kituo hicho Sister Sabina Mangi amesema ujenzi wa jengo hilo mpaka kukamilika kwake ni zaidi ya Millioni Mia sita zimetumika kukamilisha jengo hilo wakati ununizi wa vifaa umegharimu kiasi cha shilingi Milioni Mia Mbili Tisini na Tano, ambapo amesema jengo hilo limeleta ukombozi kwa akina mama kwani kwa sasa wanafanyiwa upasuaji wa dharura na upasuaji wa kawaida katika kituo hicho.
Pia ameongeza kwa kusema mbali na mafanikio hayo lakini wanakumbana na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara ambapo wameiomba serukali iweze kuwasaidi mita 900 za barabara
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Serukamba amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na taasisi za kidini kwa kutoa huduma za kijamii huku akiahidi na kuagiza kwa watendaji kuhakikisha wanakaa na kujadili na TARURA namna watakavyoondoa changamoto ya barabara inayoelekea katika kituo hicho.
"Nitoe Maagizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mumlete mtu wa TARURA aje aangalie aone tunafanya nini kuboresha barabara hii"
Nao baadhi ya wananchi wametoa shukrani nyingi sana kwa serikali na kanisa kwa kukiendeleza kituo hicho tangu kilipoanza mpaka sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza kamanda Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Iringa kufanya uchunguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kukagua Nyumba ya Mkurugenzi, hospitali ya wilaya,nyumba za watumishi Pamoja na ukarabati wa ukumbi wa siasa ni kilimo
Hayo yamejiri leo wakati wa Mhe. Serukamba alipotembelea katika Halmashauri hiyo na kukutana na madiwani na wataalamu ambapo baadhi ya madiwani wamesema kuwa kumekuwa na udanganyifu katika ujenzi wa baadhi ya maeneo.
Mhe.Mathew Singanyagwa ni Diwani wa kata wa Masaka ametoa ya moyoni na kusema kuwa suala la ukumbi wa siasa ni kilimo ni ukumbi wa muda mrefu sana na kwamba katika ukarabati wake umefikia asilimia Hamsini si sahihi na hizo nyumba za watumishi kwasasa bado ni mapagala
Mhe. Fundi Mihayo diwani wa kata ya Ilolo mpya amesema kwa sasa Halmashauri hiyo haiko vizuri sana kwani katika hospitali ya Wilaya mpaka sasa kuna majengo nane hayajakamilika na pesa tayari Serikali imekwisha kutoa hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa kulishughulikia hili suala
Nae Mhe. Yohanes Mlusi amesema kuwa wao kama madiwani ndio wasimamizi wakuu wa kuhakikisha miradi ya Serikali inakwenda lakini kumekuwa na changamoto ya wao madiwani kutosikilizwa pale wanapo shauri kwa wataalamu mambo ya kufanya
Akizungumza baada ya kuwasikiliza madiwani hao Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amesema kufikia jumatatu ya wiki ijayo anahitaji majibu kutoka kwa takukuru juu ya miradi ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ya wilaya,nyumba za watumishi,ukuta wa wigo wa jengo la Halmashauri na ukumbi wa siasa ni kilimo
“na Takukuru nataka unisaidie jambo moja tumeambiwa ukumbi huu haukarabatiwa lakini kuna hela za ukarabati zimewekwa nataka uthibitishe tunakarabati au la,nataka uniletee ripoti juu ya uzio huo ulioanguka kuhusu nyumba hiyo ya Mkurugenzi lakini pia kuhusu Hospitali ya Wilaya nataka hiyo ripoti tujue”
Aidha Mhe. Serukamba amewataka wahasibu kwenye Halmashauri kuachana na tabia ya kukaa na fedha zilizotoka Serikali kuu na badala yake amesema fedha hizo pindi zinapofika wahakikishe wanazipeleka kwenye miradi husika.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa watashughulika na wabadhirifu wote wanaorudisha maendeleo nyuma kwa kujinufaisha wao binafsi hivyo wananchi waendelee kuwa na Imani na Serikali yao.
Sambamba na hayo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Stephen Mhapa ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Mkoa na wengineo kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego Amewataka Wananchi wote Kutumia Fursa ya Maonyesho ya Utalii Karibu Kusini Yatakayofanyika Katika Viwanja vya Kihesa Kilolo Kuanzia Tarehe 23 hadi 27/09/2023.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema kuwa lengo la maonyesho hayo ni pamoja na kuiishi kampeni ya The Royal Tour ilioanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na kutangaza fursa za utalii na uwekezaji zilizopo kusini mwa Tanzania.
Mikoa Kumi ya Kusini mwa Tanzania Inataraji Kushiriki Maonyesho Hayo yenye Hadhi ya Kimataifa
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.