Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amempokea Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, ambaye amewasili Mkoani Iringa Kwaajili ya ziara ya kukagua na kuzindua Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita, ambapo leo ameanza kuzindua miradi ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Septemba 12,2024 amefunga mafunzo ya Muujibu wa sheria katika kikosi cha Jeshi 841 KJ MafingaKabla ya kufunga Mafunzo hayo Mhe. Serukamba alipokelewa na Mwenyeji wake ambaye ndiye Mkuu wa kikosi Kanali Issa Chalamila na badae akagua gwaride
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Leo Septemba 09,2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya MufindiAkiwa katika ukaguzi huo Mhe. Serukamba kwanza ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoingozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa shule za msingi na sekondari jambo ambalo linaenda kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata elimu.Moja ya mradi aliotembelea ni mradi wa shule Mpya ya Sekondari ya Kibengu ambayo ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi Millioni 583 ambapo akiwa hapo Mhe. Serukamba ameridhishwa na mradi huo ulipofikia huku akiagiza kuendelea kuongeza kasi ili majengo ya shule hiyo yaweze kukamilika kwa wakati.Nao baadhi ya Wananchi wametoa shukrani nyingi kwa Serikali kwa kuwajengea shule na kuboresha miundombinu ya shule kwa kusema kuwa miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili wanafunzi waondokane na adha ya kutembea umbali mrefu kupata elimuSambamba na hayo Mhe. Serukamba ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuwahi kuanza kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kwani kwasasa hakutakuwa na changamoto ya kukwama kwa miradi kwa kisingizio cha mvua
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.