Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa masaa 24 Kwa wafanyabiashara wanaomiliki vibanda katika soko la Mafinga kuvunja vibanda 331 vilivyojengwa kimakosa katika eneo linalomilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga ambavyo husababisha hasara ya zaidi ya Millioni Kumi Kwenye Halmashauri hiyo.Hayo yamejiri wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika soko hilo akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na MkoaMhe. Serukamba amesema kuwa Halmashauri haiwezi kuendelea endapo hakuna mapato yoyote yale yanayoingia katika Halmashauri hivyo amesema kuwa hawajalipa kodi kwa zaidi ya miezi sita basi wapishe kwenye eneo hilo la Halmashauri Hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwanza kuzungushia utepe kwenye eneo hilo ili vibanda hivyo viweze kubomolewa."Kwahiyo nimetoa maelekezo watakuja kufunga liboni tanesco wataondoa umeme ili kesho kutwa tunaanza kubomoa vibanda vyote ili tubakie na ardhi yetu halafu baada ya hapo tutajua tunalipangaje soko letu na tutaanza kufanya biashara na wale ambao watahitaji kufanya biashara na sisi"Nae Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amesema kutokana na kukosa Mkataba wafanyabiashara hao wamekosa leseni na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapatoKwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Viwanda na Biashara wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndg. Evance Mtikile suala la mgogoro wa mkataba kati ya wafanyabiashara hao na Halmashauri limeanza tangu mwaka jana ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakigomea mkataba huo na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapato.
Ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka wafanyakazi nchini kuanza utaratibu wa kujiwekea akiba kwa maisha yajayoAkizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Serukamba amewasisitiza Watanzania kwa kusema kuwa Dunia inapaswa kuiga kutoka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwa kuiga na wao kuanza kujiwekea akiba katika maisha yajayo kwenye familiaPia ameongeza kwa kuwataka wafanyakazi hao kuwa na maadili katika utendaji wa kazi wawapo Ofisini na pindi wanapowahudumia wananchi.Sambamba na hayo amewataka wafanayakazi hao kuendeleza mapambano ya kupambana na ukatili wa kijinsia na kutokomeaza
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameshiriki katika uzinduzi wa jengo la upasuaji mkubwa la kituo cha Afya cha Wenda kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kinachomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Iringa.
Katika uzinduzi wa jengo hilo zipo baadhi ya changamoto ambazo kituo hicho wanakumbana nazo kubwa ikiwemo miundombinu mibovu ya barabara ya kufikia katika kituo hicho, ambapo Mhe. Serekamba amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kukutana na Meneja wa TARURA kuhakikisha wanatengeneza Barabara hiyo.
Aidha amesema Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi za kidini katika kuhudumia jamii hivyo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini.
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.