Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa amefanya uzinduzi wa kikao cha kupokea maagizo ya Miongozo Mitatu ya Kuboresha Elimu ya Misingi na Sekondari uliotolewa Agosti mwaka huu Mkoani Tabora na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Shule ya wasichana Iringa.(Iringa gilrs) Katika uzinduzi huo Mhe Halima Dendego amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya huku akiwaahidi kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha walimu wanapatiwa haki zao za msingi na wanawajibika katika kutoa Elimu Bora. Aidha Mhe. Halima Dendego amesema “Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kila mwaka tutakuwa tunaandaa kikao cha tathimini kwa sekta ya Elimu ili tuweza kuona mafanikio,changamoto na mambo yanayofuata siku za mbele tuweza kuyakabiliwa kwa Pamoja”
Mhe Queen Sendiga akitoa maelezo ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya Mkoa wa Iringa upande wa Barabara (TARURA na TANROADS) ndani ya kipindi cha mwaka mmoja cha Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mhe Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga akitoa maelezo ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya Mkoa wa Iringa katika sekta ya kilimo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja cha Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.