Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego Amewataka Wananchi wote Kutumia Fursa ya Maonyesho ya Utalii Karibu Kusini Yatakayofanyika Katika Viwanja vya Kihesa Kilolo Kuanzia Tarehe 23 hadi 27/09/2023.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo amesema kuwa lengo la maonyesho hayo ni pamoja na kuiishi kampeni ya The Royal Tour ilioanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na kutangaza fursa za utalii na uwekezaji zilizopo kusini mwa Tanzania.
Mikoa Kumi ya Kusini mwa Tanzania Inataraji Kushiriki Maonyesho Hayo yenye Hadhi ya Kimataifa
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego ametolea ufafanuzi taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijaamii zilizojaa upotoshaji juu ya sekali ngazi ya Mkoa na wilaya kutoa maelekezo kwa watendaji kuvunja na kuharibu miundombinu ya wafanyabiashara.Mhe.Dendego ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari ambapo amesema kuwa Serikali ya Wilaya na Mkoa haihusika na zoezi hilo lililoendeshwa kwa kutokufuata maelekezo rasmi yaliyotolewa na viongozi kwa lengo la kutengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya wafanyabiashara.Pia Dendego amesema watu wote waliohusika kutoa maelekezo ya kufanya uharibifu huo na kuleta taharuki kwa wafanyabiashara watachukuliwa hatua kali za kisheria na kinidhamu.Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi kufanya kazi kwa kushirikishana ili kuleta tija na kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi.Imetolewa na Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.