Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Leo Septemba 09,2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya MufindiAkiwa katika ukaguzi huo Mhe. Serukamba kwanza ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoingozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa shule za msingi na sekondari jambo ambalo linaenda kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata elimu.Moja ya mradi aliotembelea ni mradi wa shule Mpya ya Sekondari ya Kibengu ambayo ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi Millioni 583 ambapo akiwa hapo Mhe. Serukamba ameridhishwa na mradi huo ulipofikia huku akiagiza kuendelea kuongeza kasi ili majengo ya shule hiyo yaweze kukamilika kwa wakati.Nao baadhi ya Wananchi wametoa shukrani nyingi kwa Serikali kwa kuwajengea shule na kuboresha miundombinu ya shule kwa kusema kuwa miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili wanafunzi waondokane na adha ya kutembea umbali mrefu kupata elimuSambamba na hayo Mhe. Serukamba ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuwahi kuanza kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kwani kwasasa hakutakuwa na changamoto ya kukwama kwa miradi kwa kisingizio cha mvua
Mkoa wa Iringa ambao ni kinara kwa uzalishaji wa vyakula sasa inaondokana na hali ya udumavu ambapo Mkuu wa Mkoa , Mhe. Peter Serukamba amezindua kampeni maalum ya kupima hali ya lishe kwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ambapo kwa Mkoa mzima ni watoto 2,059,204/= ili kubaini viashiria vya udumavu
Kampeni hiyo imezinduliwa na kuanza rasmi leo Juni 12,2024 katika vituo vyote vya afya vilivyo ainishwa .
Akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi Mhe. Serukamba amesema kuwa kuhusu kampeni maalam ya kutathimini hali ya lishe kwa Watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 itakayofanyika kuanzia leo mpaka Juni 15,2025 kwa Mkoa mzima.
“Kinachotakiwa kwenu Wajumbe ni kutoa hamasa katika jamii, kusimamia shughuli za kampeni,kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kufikia maendeleo na kufanikisha zoezi la ufanyaji wa tathmini ya hali ya lishe kwa Watoto Mkoani Iringa na kuepusha upotoshaji wowote utakaoweza kujitokeza lakini pia Wajumbe wa kamati hii mnapswa kuhakikisha mnakanusha taarifa za upotoshaji unaoweza kujitokeza katika kampeni hii ”
Kwa upande wake Afisa lishe wa Mkoa wa Iringa ,Anna Nombo amesema timu ya Wataalam 343 kwa Mkoa watafanya vipimo ili kutathimini hali ya lishe na kupima kimo au urefu, uzito pamoja na mzingo wa kati wa sehemu ya juu ya mkono,kuangalia hali ya chanjo, kuangalia uwepo wa uvimbe mbonyeo katika miguu yote miwili , uwepo wa magonjwa sugu,ulemavu , hali ya ukamilishaji wa umezaji wa dawa za minyoo na kutambua uelewa wa malezi ya watoto.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa baada ya mtoto kupimwa , mtoa huduma atatakiwa kufanya tafsiri ya hali ya lishe ya mtoto husika ndipo mtoto atakayekutwa na hali duni ya lishe mzazi wake atatakiwa kufatiliwa namna ya malezi yake na ulishaji wa mtoto wake kupitia dodoso maalum ili itakapofikia hatua ya utatuzi kuweza kuitatua changamoto hiyo.
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.