Zaidi ya washiriki 10,000 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya kitaifa ya michezo kwa shule za msingi na sekondari, UMITASHUMTA na UMISSETA, yatakayofanyika mkoani Iringa kwa mara ya kwanza mwaka 2025, tukio linalotajwa kuwa la kihistoria kwa Mkoa wa Iringa .Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba, amethibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mashindano hayo ni fursa adhimu kwa mkoa wa Iringa, huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiamini Iringa kuwa mwenyeji wa tukio hilo la kitaifa.“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutupatia heshima hii kubwa, Kwa mara ya kwanza Iringa itakuwa mwenyeji wa mashindano haya makubwa, baada ya kuwa yamefanyika mkoani Tabora kwa mfululizo Kwa miaka mitatu ,” amesema Mhe. Serukamba.Kwa mujibu wa ratiba rasmi, mashindano ya UMITASHUMTA yataanza tarehe 08 Juni hadi 17 Juni 2025, yakifuatiwa na mashindano ya UMISSETA yatakayodumu kuanzia tarehe 08 hadi 30 Juni 2025.Mashindano hayo yanatarajiwa kukutanisha wanafunzi, walimu wa michezo, maafisa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka sekta ya elimu na michezo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, netiboli, pamoja na mchezo wa kengele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Aidha, burudani ya muziki wa kizazi kipya pia itakuwepo, ikitumbuiza na kuhamasisha washiriki na mashabiki.Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni pamoja na Shule ya Sekondari Wasichana Iringa, Shule ya Sekondari Lugalo, pamoja na Chuo cha Ualimu Klerru.Aidha Mhe. Serukamba amewataka wananchi wa Iringa kutumia vyema fursa hii kwa kutoa huduma mbalimbali zitakazowawezesha kunufaika kiuchumi.“Wananchi wanayo nafasi ya kipekee ya kunufaika na wageni watakaofika hapa. Huduma za malazi, vyakula, usafiri na biashara ndogondogo zote zitahitajika. Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia ufunguzi rasmi wa mashindano hayo utakaofanyika tarehe 09 Juni 2025
Ikiwa ni mwendelezo wa ziara za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Januari 27, 2025 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kufanya Mkutano wa hadhara Kijiji cha Itunundu, tarafa ya Pawaga huku akiwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidiiAkizungumza wakati wa mkutano huo na wanakijiji Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa changamoto zote zilizowasilishwa na wanakijiji zitafanyiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo huku akiwataka wanakijiji wa Itunundu kufanya kazi kwa Bidii kupitia miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo."Niwaombe mfanye kazi kwa bidii Serikali inawekeza kwenye umwagiliaji, Serikali inawekeza kwenye mashule inawekeza kwenye umeme, inawekeza kwa kila kitu lakini kama wewe mmoja mmoja hufanyi juhudi bado tutaendelea kuilaumu Serikali wakati Serikali imefanya kila kitu."Sambamba na hayo Mhe. Serukamba ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa namna walivyopambana katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amehimiza Wazazi na Walezi Nchini kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu na kuwahimiza watoto hao juu ya Umuhimu wa Elimu kwani Elimu ndio Nguzo ya maendeleo ya jamii na UchumiAmeyasema hayo leo Septemba 20,2024 wakati akihutubia kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule ya Real Hope iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi.Mhe Serukamba Amesema kuwa jambo kubwa ambalo watoto wanatakiwa kurithi kutoka kwa wazazo wao ni Elimu hivyo wazazi wametakiwa kulipa kipaumbele suala la elimu ili kuleta maendeleo katika jamiiAidha Mhe. Serukamba ameongeza kwa kuwataka wasomi wote kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwa kusoma vitabu mbalimbali kwani kwa sasa sayansi na Teknolojia ikekuwa kwa kasi tofauti na hapo awali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.